Uncategorized

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa watekwa na Serikali ya Uganda


Mwandishi: Robert Matovu
Uhasama wa serikali ya Uganda dhidi ya raia Rwanda umezidi. Katika hali isiyo ya kawaida, Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) limesitisha kusafirisha Majeshi, polisi na raia kutoka Rwanda kupitia Uganda. Kutokana na gazeti la Virungapost.com, hatua hii imechukuliwa baada ya kutekwa na kuteswa kwa wafanyakazi wawili wa UN ambao ni raia wa Rwanda.
Kutokana na habari za kuaminika wafanyakazi hao wa Umoja wa mataifa walitekwa na mashushushu wa Idara ya ujasusi wa kijeshi wa Uganda (CMI). Wafanyakazi hao ni Francis Bihoyiki aliyekamatwa tarehe 13 Juni 2019, ambaye ni mfanyakazi wa UN katika kambi ya wakimbizi ya Kyaka, magharibi ya mji mkuu Kampala. Mwingine ni Antoine Musinga aliyenyakuliwa na maajenti wa CMI tarehe 26 Juni. Huyu Musinga ni mtumishi wa UN kituo chake cha kazi kipo Entebbe.
Kukamatwa kwao kunaitwa kutekwa, kwa kuwa kulifanywa kinyume cha sheria, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na chombo kisicho na mamlaka ya kisheria kufanya hivyo (kwa hali ya kawaida Jeshi la Polisi ndilo lina mamlaka hayo), kuwafungia mahali pasipojulikana na baadae kuwatesa, kutofikishwa mahakamani kama kuna tuhuma dhidi yao na kadhalika.
Hatua hii ya Umoja wa Mataifa, inafuata ile iliyochukuliwa na serikali ya Rwanda mwezi Machi 2019, ya kuwashauri wananchi wake kuacha kwenda nchini Uganda kwa sababu za kiusalama. Nchi ya Rwanda ilichukua msimamo baada ya mamia ya raia wake kukamatwa, kusafirishwa huku wamefungwa kitambaa machoni, kuteswa, kufungwa kwa muda mrefu kinyume cha sheria, na kuporwa mali zao nchini Uganda.
Baadhi yao, wanaobahatika, hutupwa mpakani na CMI wakiwa wamedhoofika na wana maumivu yaliyokithiri. Wanaorejeshwa katika hali hiyo wanasema kuna wengi kwa mamia wanabaki kwenye gereza za Uganda, na karibu ya wote wanadai huhamasishwa kujiunga na kikundi cha magaidi cha Rwanda National Congress (RNC) kinachoongozwa na Faustin Kayumba Nyamwasa ambaye anaishi nchini Afrika ya Kusini. Wakikataa wanafungwa kwa muda mrefu kwa tuhuma zisizo na mashiko kuwa ni wapelelezi wa Rwanda.
Kundi hili la RNC linashutumiwa kuhusika na mashambulio ya magruneti nchini Rwanda mwaka 2012. Nchi ya Rwanda inaishutumu Uganda kuwasaidia RNC, na wakati wote shutuma hizi huambatana na ushahidi. Mara kadhaa serikali ya Rwanda imeiomba Uganda kuwafikisha mahakamani wale wanaokamatwa lakini hakuna hata mmoja ambaye kashitakiwa.
Ukatiri huu wa kuwakamata watu kiholela, kuwatesa na kuwaua maelfu, unatukumbusha sisi wananchi wa Uganda, enzi za Dikteta Idd Amin na kundi lake la State Research Bureau (SRB). Vikosi vya SRB, vilikuwa vilijiweka juu ya sheria na viliuwa watu wengi sana. Mtindo huu ndio umeshamiri Uganda chini ya uongozi wa Yoweri Kaguta Museveni ambaye alishirikiana na Jeshi la Tanzania kumng’oa Amin.
Makundi yanayopewa msaada na Uganda ni pamoja na lile la FDLR, ambalo ni kundi la Wahutu wenye itikadi ya mauaji ya kimbari, na ambao viongozi wake walihusika katika mauaji ya kuangamiza Watusi mwaka 1994. Ripoti iriyoaandaliwa na jopo la wataalamu la Umoja wa Mataifa na kutangazwa tarehe 31 Desemba 2018, iliainisha kuwa kuna makundi yanayojiita P5 yakiwemo RNC, FDLR, FDU-Inkingi na MRCD yanayotafuta wafuasi kupitia Uganda na Burundi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: