Uncategorized

Acheni kwenda Uganda. Rusa na Maniraguha wawashauri Wanyarwanda

Mwandishi: Robert Matovu

Yeyote anayekumbuka historia ya Uganda wakati wa Dikteta Idd Amin Dada, hawezi kusahau jinsi wananchi walivyokuwa wanakamatwa, kufungwa vitambaa machoni na kutupwa kwenye buti za magari na makachero wa State Research Bureau (SRB).

Leo hii, hayo ndiyo yanayowapata Raia wa Rwanda wanapokwenda Uganda kwenye biashara zao au kuwasalimia ndugu na marafiki zao. Kukamatwa huko kinyume cha sheria, kuporwa mali, mateso ya mwili na kisaikolojia, na wanaobahatika kutupwa mipakani, kumewakumba mamia kama si maelfu ya Raia wa Rwanda kuanzia mwaka 2017.

Usidhani ni SRB inayofanya hayo, bali Idara ya ujasusi wa kijeshi wa Uganda (CMI). Idara ambayo chini ya uongozi wa Rais Yoweri Museveni, imekwezwa juu ya vyombo vingine vya dola.

Rene Rutagungira alichukuliwa mithiri ya kutekwa na maajenti wa CMI tarehe 7 Agosti 2017. Mpaka sasa yuko kwenye mahabusu ya kijeshi ambapo haki zake za binadamu haziheshimiwi. Anateswa na kufanyiwa vitendo vingi viovu, kukiwemo jeshi la nchi hiyo kushindwa kumfikisha mbele ya mahakama.

Rutagungira alinyakuliwa na CMI kutoka kwenye baa moja kwenye kitongoji cha Bakuli, jijini Kampala alipokuwa akifurahia kinywaji na marafiki zake. Alijalibu kupiga mayowe ilia pate msaada lakini haikuzaa matunda.

Watekaji wake walimpeleka na kumfungia kwenye mahabusu ya Makao Makuu ya CMI yaliyopo eneo la Mbuya. Alikaa hapo kwa siku kama si miezi kadhaa kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi ya kijeshi iliyopo Makindye.

Rutagungira amekuwa mkazi wa mahabusu hayo kwa miaka karibu miwili sasa, bila ya idhini au uhuru wa kutembelewa na familia yake, au kupewa huduma za kibalozi na Ubalozi wa Rwanda nchini Uganda.

Akiwa korokoroni kwenye hiyo kambi ya kijeshi ya Makindye, Wakili aliyeruhusiwa kumwona anathibitisha kuwa Rutagungira aliteswa. Mateso aliyoyapata ni mengi kukiwemo kupigwa sehemu nyingi za mwili na kupigwa shoti za umeme. Yote hayo yakiwa ni njia ya kumfanya akili kuwa ni jasusi wa serikali ya Rwanda.

Katika watu wanaoshutumiwa na mhanga kuwa walimtesa, ni pamoja na Jemadari Henry Tumukunde ambaye hivi karibuni alikuwa ni Waziri wa Usalama wa Taifa wa Uganda.

Mwezi Mei 2019 Rutagungira alifikishwa mbere ya mahakama ya kijeshi (Makindye General Court Martial) na wakashindwa kutoa ushahidi dhidi yake. Wakili wake aliomba aachiwe huru kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo kikatiba wa kusikiliza kesi ya raia (civilians). Waendesha mashtaka wa Jeshi la Uganda walipuuza kinachotajwa na Katiba ya nchi hiyo hususani ibara ya 210 na ya 126.

Uganda imekuwa kitovu cha makundi ya kuihujumu Rwanda na makundi mengi yakiwemo

lile la FDLR, ambalo ni kundi la Wahutu wenye itikadi ya mauaji ya kimbari, na ambao viongozi wake walihusika katika mauaji ya kuangamiza Watusi mwaka 1994. Ripoti iriyoaandaliwa na jopo la wataalamu la Umoja wa Mataifa na kutangazwa tarehe 31 Desemba 2018, iliainisha kuwa kuna makundi yanayojiita P5 yakiwemo RNC, FDLR, FDU-Inkingi na MRCD yanayotafuta wafuasi kupitia Uganda na Burundi.

Waliorudishwa waonya

Mwezi machi mwaka huu serikali ya Rwanda iliwaonya raia wake kuhusu hali ya usalama wa Wanyarwanda wanauzuru Uganda. Baadhi ya wale waliofikiri ni mzaha, leo hii ndio wanathibitisha kuwa kweli ni hatari.

Tarehe 3 Julai, gazeti la The New Times lilichapisha makala ya habari kuhusu wanyarwanda wawili waliotupwa na serikali ya Uganda kwenye mpaka wake na Rwanda. Hao ni Celestin Maniraguha, mwenye umri wa miaka 39, na Moses Rusa mwenye umri wa miaka 64.

Baada ya siku kuu ya Pasaka Maniraguha alisafiri kwenda Kisoro Uganda kwenye kazi yake ya ufyatuaji wa matofali. Alivyofika Kisoro alimdai bosi wake malipo ya kazi aliyokuwa ameifanya kabla ya kurudi Rwanda kusherehekea pasaka. Badala ya kulipwa, huyo boss wake alikwenda Polisi na kudai kwake kuna jasusi la Rwanda.

Maniraguha alikamatwa akafungiwa sehemu zisizojulikana kwa kuwa hakufungiwa kituo cha Polisi.  Alifungiwa Kisoro na baadaye Mbarara kabla ya kuhamishiwa makao makuu ya CMI jijini Kampala. Alikaa korokoroni huku akiteswa kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu kabla ya kutupwa kwenye mpaka wa Uganda na Rwanda.

Moses Rusa, alikamatwa wakati anapanda basi kurudi Rwanda. Rusa alikuwa anatoka Rwentobo, Kusini-Magharibi mwa Uganda alipokwenda kumtembelea baba yake mdogo mwenye umri wa miaka mia moja (100). Rusa alivuka mpaka kwenda Uganda tarehe 26 Juni, 2019.

Baada ya kukamatwa, Rusa alisafirishwa kwa karibu kilomita 500 hadi Kampala kwenye Makao Makuu ya CMI. Na yeye pia anasimulia alivyotekwa, akateswa, akaitwa jasusi na kadhalika.

Rusa na Maniraguha wanawaasa wananchi wa Rwanda kujiepusha na kwenda Uganda kwani ni hatari. Wote wawili wanasema ni bora kuvuta subira mpaka hapo hali ya kawaida itakaporejea. Hali hiyo, ni pale Rais Museveni atakapoacha kuwakamata ovyo Raia wa Rwanda na kuacha kuvisaidia vikundi vya waovu, chini ya mwavuli wa P5.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: