Uncategorized

Mhimili wa Kongo-Angola-Rwanda umeanza kuzaa matunda

Mwandishi: Robert Matovu


Amani na usalama wa nchi za eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, ni swala ambalo limepewa kipaumbele. Tarehe 12 Julai 2019, Jijini Luanda, ulifanyika mkutano wa kilele uliowahusisha marais João Lourenço wa Angola, Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paul Kagame wa Rwanda, na Yoweri Museveni wa Uganda.
Katika yaliyozungumzwa ni pamoja na kuwepo kwa makundi yenye silaha Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kudorora kwa uhusiano kati ya Rwanda na Uganda. Makundi hayo mara nyingi pamoja na kuyumbisha usalama wa raia nchini Kongo, yameigeuza nchi hiyo kama uwanja wa kuziyumbisha nchi zao.
Kuboreshwa kwa uhusiano kati ya Luanda, Kinshasa na Kigali inaonekana kuwa ni chanzo cha mkutano huu wa kilele. Kuwa madarakani kwa marais Tshisekedi na Lourenço kumeleta mwelekeo mpya wa siasa kati ya nchi hizi tatu.
Mwishoni mwa mwezi Mei 2019, wakuu wa nchi za Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda walitia sahihi mkataba muhimu katika maswala ya uchumi na kurejesha usalama katika nchi hizi.
Katika makubaliano hayo walikubaliana kushirikiana katika kile kilichoitwa “Mhimili wa Kongo-Angola-Rwanda” kuyafyeka makundi yanayovuruga usalama wa nchi zao ambayo yameigeuza Kongo uwanja wa mapambano na hujuma.


Aidha mkataba huo ulibainisha mpango wa kuifufua kwa kuikarabati reli ya Kolwezi-Dololo yenye urefu wa kilometa 422 na kuliunganisha eneo la Kusini-Magharibi mwa Kongo na jimbo la Benguela magharibi mwa Angola.
Katika makubaliano hayo, wakuu hao wa nchi tatu walikubaliana kuwahusisha wakuu wengine wa nchi kwenye ukanda huu wa maziwa makuu kwa lengo la kutekeleza mpango huu wa kuyateketeza makundi ya kigaidi. Kutiwa sahihi kwa makubaliano hayo kulifuatiwa na kuzitokomeza kambi mbili (nchini Kongo) za kundi la kigaidi la Rwanda National Congress (RNC) linaloongozwa na Kayumba Nyamwasa.
Mwezi Desemba 2018, jopo la wataaalam wa Umoja wa Mataifa lilichapisha ripoti iliyobainisha kuwa Uganda ndiyo makao makuu ya muungano wa makundi yaliyo chini ya mwavuli ujulikanao kama P5, ukiwa na mpango wa kuihujumu nchi jirani ya Rwanda.
Huo mwavuli wa P5 inajulikana kuwa unapata msaada wa hali na mali kutoka kwenye serikali ya Uganda, hususani kwa Rais Yoweri Museveni na Idara ya ujasusi wa kijeshi wa Uganda (CMI). Uratibu wa P5 unayahusisha makundi kama magaidi wa RNC, na pia FDLR, FDU-Inkingi na MRCD yanayojulikana kwa kuwa na itikadi ya mauaji ya kimbari.
Pamoja na uratibu na uhamasishaji wa kutafuta wafuasi kupitia Uganda na Burundi, mapema mwaka huu wa 2019, Rais Museveni alikili kuwapokea na kuwa na mazungumzo na viongozi wa RNC Charlotte Mukankusi, Tribert Ayabatwa Rujugiro na Eugene Gasana. Mukankusi anakaa nchini Kanada wakati Gasana anakaa Marekani.


Huyu Mukankusi ambaye ni binamu yake Kayumba Nyamwasa, alipewa pasipoti ya kusafiria na Idara ya Uhamiaji ya Uganda kwa amri ya Rais Museveni. Pasipoti hiyo mpya yenye No. A00019997 ilitolewa tarehe 11 Februari 2019 na itamaliza muda wake tarehe 10 Februari 2024.


Mhimili huu wa Kongo-Angola-Rwanda, umeanza kuzaa matunda ikiwa ni pamoja na kulizungumzia swala la uhusiano mbaya wa Rwanda na Uganda, ambao chanzo chake ni Rais Museveni na mdogo wake Salim Akandwanaho Saleh.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: