Uncategorized

Hija ya Yoweri Museveni Chato ni Unafiki Mkubwa

Mwandishi: Robert Matovu
Ikiwa ni siku moja tu baada ya mkutano wa kilele wa marais João Lourenço wa Angola, Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paul Kagame wa Rwanda, na Yoweri Museveni wa Uganda, Tanzania ilipata ugeni wa ghafla.
Rais Museveni alikutana na mwenyeji wake Rais Pombe John Magufuli, nyumbani kwake Chato. Akiwahutubia wananchi waliomlaki katika ugeni huo, Rais Museveni alitangaza kuwa alikuwa amekwenda Tanzania kama hija. “Wakristo wanakwenda kuhiji Roma, na Waislam kwenda kuhiji Mecca, mimi hija yangu ya kisiasa ni Tanzania”.
Hotuba yake aliyoitoa kwa Kiswahili ilishangiliwa sana, ilikuwa ni unafiki uliokithiri. Ni kweli kuwa Rais Museveni alisomea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam enzi za uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wakati huo Tanzania ilikuwa ni nchi ililiyokuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa bara letu la Afrika.


Viongozi kama Samora Machel wa Msumbiji, Sam Nujoma wa Namibia na Museveni wa Uganda waliishi na kupata uzoefu katika mapambano nchini Tanzania. Vyama vilivyoendesha vuguvugu la ukombozi kama ANC ya Afrika ya Kusini, SWAPO ya Namibia, ZANU-PF ya Zimbabwe vilipata msaada mkubwa wa Tanzania. Ukombozi wa Uganda dhidi ya utawala wa Iddi Amin ulifanywa na Tanzania kwa gharama kubwa.
Hotuba ya Museveni na hija yake nchini humo, nasema ni unafiki kwa kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa mtu mwenye uchu uliozidi wa mali na madaraka. Mwalimu Nyerere aliiunganisha nchi na kuipenda Afrika bila kipimo. Kama ni hija kweli Rais anastahili kutubu.


Katika historia yake Mwalimu Nyerere aliyeiaga dunia karibu miaka 20 iliyopita, alipiga vita ufisadi katika utawala wake wote. Mwalimu aliamini rushwa ni adui wa haki. Imani hiyo ndiyo ya Rais Pombe Magufuli, ambaye utawala wake umeigeuza Tanzania mfano wa kuigwa katika kupiga ufisadi.
Hayo yote ni kinyume sana na sera za Museveni na familia yake. Kila kitu kilichopo Uganda anataka kimilikiwe na familia yake. Kama si yeye, ni mkewe. Kama si mke wake ni mashemeji (kaka za mkewe) au watoto wake. Kama si hao ni mdogo wake Salim Saleh na mkewe Jovia Akandwanaho. Familia yake ina utajiri mkubwa kiasi ambacho hakielezeki. Ni katika kutetea utajiri huo, wameanzisha makundi ya wanamgambo wa kuwateka watu na kuwapora.


Wanasiasa chipukizi kama Robert Kyagulanyi ajulikanaye kama Bobi Wine wanaodiriki kusema imetosha, maisha yao yako hatarini kwani hili genge la mafia haliwezi kukubali mabadiriko.
Wachunguzi wa mambo wanaamini uhasama alio nao Rais Museveni dhidi ya Rwanda, unatokana na wivu. Wivu unaotokana na sifa za Rais Paul Kagame kupiga vita ubadhilifu wa mali ya umma, vita dhidi ya ufisadi na ukandamizaji. Utawala wa Kagame umekuwa wa kuigwa lakini haimfurahishi Museveni ambaye hapendi kiongozi mwingine asifiwe hata kama anastahili.
Hizo sera zinazoleta mabadiliko chanya, ndizo zimesababisha Museveni awaung mkono na kuwasaidia magaidi wa kundi la Rwanda National Congress (RNC) na FDLR. Wakiwa Angola, naamini yote haya aliambiwa. Badala ya kuyatafakali akaomba Waganda wamsamehe, anazidi kukaza Kamba aliyowafungia.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: