Na: Robert Matovu
Serikali ya Rwanda imekuwa ikiishutumu ile ya majirani zake wa kaskazini ya Uganda, kuwaunga mkono kwa hali na mali makundi ya waasi wanaoihujumu. Makundi hayo ni pamoja na lile la kigaidi la Rwanda National Congress (RNC), na lile la FDLR lenye viongozi wanaoshutumiwa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994. Kuna ushahidi mkubwa kuthibitisha madai haya ya Rwanda.
Shutuma kama hizo dhidi ya serikali ya Rais Yoweri Kaguta Museveni kuwaunga mkono waasi zimetolewa na serikali ya Sudan Kusini. Shutuma hizi mpya dhidi ya Uganda kuwaunga mkono waasi wa jirani yake wa kaskazini zilitolewa na viongozi wa mikoa inayopakana na Uganda tarehe 19 Julai 2019. Mkutano hupo uliowakutanisha viongozi wa Uganda na Sudani kusini, ulifanyika kwenye makao makuu ya wilaya Maqwi.
Katika mkutano huo, Bwana Alberio Tobiolo Oromo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Torit State na Eastern Equatorial alidai wana habari za kuaminika kuwa waasi wanazitumia kambi za wakimbizi zilizopo nchini Uganda kama uwanja wa kuaandaa mashambulizi dhidi ya Sudan Kusini. Wilaya hizo za Uganda ni Adjumani, Kiryandongo na Lamwo.
Katika mkutano huo Bwana Tobiolo alielezea tukio la hivi karibuni ambapo waasi wa Sudan Kusini walivishambulia na kuteketeza vituo vya Ofisi ya Uhamiaji na kituo cha kuchunguza ugonjwa wa Ebola vilivyopo kwenye kijiji cha Owiny Ki Bul. Washambuliaji walijifanya ni Wasudan waliokuwa wanatoka harusini.
Mkuu wa wilaya ya Magwi, Bwana Bosco Ochola Oringa alisema mashambulizi hayo ya watu wanaodhaniwa kuwa waasi, hivi karibuni walivilenga vijiji vya Adodi, Owiny Ki Bul, Mugale na Paracelle. Waasi hao hufanya mashambulio kati ya barabara inayoiunganisha miji ya Nimule na Juba, mara nyingi wakiwavamia na au kuwaua raia wa kawaida, kitu ambacho kimesababisha wasiwasi mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Bwana James Nabinson Kidega aliyeiwakilisha serikali ya Uganda hakukanusha au kuthibitisha malalamiko ya jirani. Hahuweza pia kuto ufafanuzi wowote, bali kuahidi kuwa nchi yake itafanya uchunguzi wa kina dhidi ya madai hayo.
Inavyoonekana ni sera ya Uganda kuwayumbisha majirani zake hasa wale anaowadhania ni wanyonge kwake japo wanajua wazi kuwa kulinda uhuru wa nchi siyo jambo la mzaha.