Uncategorized

Baada ya Mbonimpa kurejeshwa na 40 kukamatwa, Rwanda inaiomba Uganda Maelezo

Baada ya Mbonimpa kurejeshwa, 40 kukamatwa Rwanda inaiomba Uganda Maelezo
Mwandishi: Robert Matovu
Serikali ya Rwanda imeiomba serikali ya Uganda kuifahamisha nini kinaendelea baada ya wananchi wake wengine kukamatwa. Alhamisi ya tarehe 25 Julai, Balozi wa Rwanda nchini Uganda, Frank Mugambage, rasmi aliiomba Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje Kampala kupewa maelezo ya kulikoni kuna wimbi jipya la kamata kamata.


Baada ya mkutano wa kilele wa Marais nchini Angola tarehe 12 Julai 2019 kulivuma upepo wa matumaini kuwa hali itarudia kuwa ya kawaida kati ya Uganda na Rwanda. Viongozi hao wa nchi, João Lourenço wa Angola, Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paul Kagame wa Rwanda, na Yoweri Museveni wa Uganda, kwa undani walizungumzia malalamiko ya Rwanda kuhusu jirani yao wa Kaskazini.


Hayo yote yangewezekana iwapo kungekuwa na utashi wa kisiasa wa Rais Museveni wa Uganda ambaye mpaka sasa haonyeshi kubadili msimamo wa kuwakamata, kuwatesa, kuwafunga na kuwapora raia wa Rwanda wanaokwenda nchini huko kwa sababu za kijamii na kibiashara.
Kukamatwa kwa Wanyarwanda 40
Jumanne ya tarehe 23 Julai 2019, mchana, waumini arobaini wa Kanisa lijulikanalo kama ADEPR, walikamatwa na Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Uganda/Uganda’s Chieftaincy of Military Intelligence (CMI) na kama kawaida wakapelekwa kwenye mahabusu ya kijeshi.


Watu walioshuhudia tukio hilo wanadai kuwa aumini hao walinyakuliwa kutoka kwenye kanisa lao kwenye kitongoji cya Kibuye jijini Kampala. Baada ya kutolewa kanisani humo, walipandishwa kwenye magari ya kawaida ya abiria na magari matatu ya polisi yajulikanayo kwa jina la “Panda gari”.


Kutokana na magazeti kadhaa ya Uganda likiwemo lile la kwenye mtandao, linaloendesha na CMI, ‘CommandPost’ yalidai waliokamatwa ni majasusi wa Jeshi la Rwanda. Hiki ni kisingizio cha wote waliokamatwa na kuteswa Uganda.


Taarifa za mwanzo za polisi zilikariri zikisema CMI iliwaambia kuna majasusi wa Rwanda ambao walikuwa wamekusanyika katika kanisa hilo la ADEPR kupewa maelekezo na kiongozi wao mpya ambaye hajatajwa jina. Baadaye ikadaiwa Wanyarwanda hao walikuwa Uganda kwa njia zisizo halali, na kuwa walikuwa na vitambulisho vya kugushi vya raia wa Uganda.


Gazeti moja la kwenye mtandao la ‘Virungapost’ lenye uelewa mkubwa wa maswala haya linadai kukamatwa huku kunatokana na ushirikiano wa Serikali ya Uganda na kundi la kigaidi la Rwanda National Congress (RNC) linaloongozwa na Kayumba Nyamwasa anayeishi Afrika ya Kusini.
Tukio hili kwa watu hawa 40, ni mfululizo wa vitendo vya kunyakuliwa, kufungwa kinyume cha sheria, kuteswa na mengineyo mabaya wanayotendewa Wanyarwanda nchini Uganda ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miaka miaka miwili sasa.
Ni aibu
Mtu yeyote anayetumia mantiki, na anayejua ujasusi ni nini na unafanywaje, hawezi kuamini kuwa uongo huo dhidi ya hao arobaini waliokamatwa kuwa ni majasusi. Majasusi gani wanaweza kwenda kwenye mkutano kama huo kwa idadi hiyo na muda huo? Watakuwa ni wapumbavu kiasi gani kufanya ujasusi wakijua wana vitambulisho vya kugushi? Kama kweli walifanya kosa la jinai la kugushi vitambulisho, ni kwa nini wakamatwe na wanajeshi na siyo polisi? Hili la kukamatwa na wanajenshi, na msemaji wa polisi wa Uganda alionekana kukerwa na kusema wao (polisi) walitoa usaidizi tu.


Tarehe 23 Julai, siku walipokamatwa arobaini wa Kampala kijana Joseph Nzabonimpa mwenye umri wa miaka 25, alirudishwa Rwanda baada ya kukaa rumande miezi mitano (5). Akizungumuza na vyombo vya habari baada ya kurejeshwa kinyume cha sheria. Yaliyompata, na yanayowasibu Wanyarwanda zaidi ya ishirini aliowakuta katika gereza ya Wilaya ya Kisoro magharibi mwa Uganda, yanatia huzuni kwa wenye moyo na aibu kwa serikali inayoyafanya hayo.
Ilikuwa siyo mara ya kwanza kwa Mbonimpa kwenda Uganda na kufanya biashara ndogo ya kutengeneza na kuuza sambuaa akishirikiana na mw…

1 comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: