Uncategorized

Rais Museveni anaihujumu Afrika ya Mashariki Mwandishi

Robert Matovu


Mara nyingi, Rais Yoweri Kaguta Museveni amejitokeza, kwa maneno kuwa mstali wa mbere kutaka kuwepo na Shirikisho la Afrika Mashariki na muungano wa kisiasa. Lakini, anayoyatenda ni kinyume au yanakinzana na matendo. Rais Museveni anajua wazi kuwa Mkataba wa Afrika Mashariki wa soko la pamoja, hauhusu tu bidhaa bali pia kulegezwa kwa masharti kwa usafiri wa watu na upatikanaji wa ajira na huduma katika mataifa ya Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan ya Kusini na Tanzania.


Ni jambo la aibu na la kusikitisha kuona serikali ya Uganda inageuka au inageuzwa kuwa kama genge la majambazi. Ukatili wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Uganda dhidi ya raia wa Rwanda, unarejesha kumbukumbu za utawala wa dikteta Idd Amin Dada.


Augustine Rutayisire na Emmanuel Rwamucyo ni raia wa Rwanda ambao wamekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Yaliyowakuta Rutayisire na Rwamucyo ambao ni wafanyabiashara hayasemeki. Mara ya kwanza walifunguliwa mashtaka ya kuhusika na njama kwenye ujambazi wa kutumia silaha. Baadaye wakashtakiwa kuwa na silaha kinyume cha sheria. Yote haya yakiwa ni uongo na uzushi kuficha ujambazi waliofanyiwa.


Yaliyowasibu hawa wawili, yalianza pale walipokuwa wanaelekea kwenye benki moja ya biashara mjini Mbarara kuweka shillingi millioni 140 za Uganda. Walikamatwa na Mukama Moses Kandiho ambaye ni Afisa wa Usalama wa Ndani au Government Internal Security Officer (GISO) wa wilaya ya Mbarara.)


Baada ya kuwakamata, Moses Kandiho alimtaka Meja Mushambo ambaye Naibu ni mkuu wa counter-intelligence wa Divisheni ya pili ya jeshi la Uganda kuja kushiriki katika ujambazi huo.


Ikumbukwe kuwa Huyu Moses Kandiho ni mdogo wake Brigadier Abel Kandiho ambaye ni mkuu wa idara ya Ujasusi wa Kijeshi wa Uganda. Kwa kimombo ni Uganda Chieftaincy of Military Intelligence (CMI). Brigedia Jemadari Kandiho ni mratibu mkuu wa vitendo vya kuwakamata, kuwatesa, na kuwafunga bila mpango raia wa Rwanda. Pia huyu Kandiho ndiye ameshika hatamu za kukisaidia kikundi cha kigaidi chaRwanda National Congress (RNC) la Kayumba Nyamwasa.


Meja Mushambo aliwasiri akiwa na maaskari kadhaa wenye bunduki na silaha nyingine kama magruneti. Baadhi ya bunduki hizo na magruneti yaliwekwa kwenye gari la Rwamucyo na Rutayisire kama kisingizio. Kilichofuata ilikuwa ni kuwanyanganya fedha zote walizokuwa wanapeleka benki na nyinginezo halafu wakawapeleka mahabusu kwa shitaka la kuwa kwenye njama ya ujambazi na kuwa na silaha kinyume cha sheria.


Baada ya kuwafunga kwa siku kadhaa hapo Mbarara, Rwamucyo na Rutayisire walihamishiwa kwenye gereza ya Luzira iliyoko Kampala. Mwezi Mei mwaka huu, mke wa Rutayisire, Betty Mutamba, aliliambia gazeti la Virungapost kuwa mumewe alinusurika kuuawa gerezani baada ya kupewa chakula chenye vipande vidogo sana vya chupa. Alikimbizwa hospitalini na akasafishwa na akaweza kuusalimika.


Mbinu hizi za ukatili na unyanganyi unaofanywa na vyombo vya dola la Uganda, zinafanywa kwa ushirikiano wa CMI na kundi la ujasusi la RNC. Mnyarwanda anayehamasishwa kujiunga nao, akikataa anabandikwa makosa kibao ya jinai kukiwemo “kuingia nchini kinyume cha sheria”; “ kuishi nchini kinyume cha sheria”; “ujasusi” na “kuwa na silaha…”
Kati ya hao watuhumiwa wote, hakuna anayekamatwa kwa mujibu wa sheria, hupakiwa kwenye magari na kusafirishwa huku wakiwa wamefungwa vitambaa machoni, kufungiwa kwenye sehemu zisizokubalika na kutoruhusu watu kuwatembelea kukiwemo Ubalozi wa Rwanda nchini humo, na mateso yanayozidi unyama. Ni udhalimu usiosemeka.


Wanyarwanda wengi wanaokamatwa karibu ya wote hakuna anayefikishwa mahakamani kwa sababu hakuna ushahidi wa kutosha kufanya hivyo. Mwenye bahati hurundikwa kwenye gari na kutupwa mpakani.


Mwezi Januari mwaka huu, mfanyabiashara Darius Kayobera na mkewe Claudine walitekwa na maajenti wa CMI na kufungiwa kwenye mahabusu ya kijeshi ya kambi ya Mbuya jijjini Kampala. Kama kawaida, pamoja ya kuwashutumu kuwa ni majasusi wa Rwanda hawajafikiswa mahakamani na wameweka marufuku ya kutembelewa na ndugu, jamaa na marafiki.
Familia hii ya Kayobera imewaacha watoto wenye umri wa miaka 9, 6 na 3 bila ya huduma ya wazazi. Hawafikishwi mahakamani kwa sababu ya kukosa ushahidi.


Wahanga wa sera hizi za ukatili zimewaacha mamia ya wanyarwanda wakikaa jela kwa muda mrefu pasipo kujali haki zao za binadamu. Kwa mfano, Jean De Dieu Niyonteze, Rene Rutagungira, Peter Siborurema, Bernard Kwizera na David Twahirwawako gerezani kwa zaidi ya miaka miwili kinyume cha sheria. Waliteswa, walinyimwa haki ya utetezi wa mawakili na kadhalika.


Kutokana na matukio haya ya kidhalimu Rwanda iekuwa ikitoa malalamiko yake kwa Rais Museveni ambaye huyafumbia macho tu. Kwa hili, Museveni hastahili tena kujifanya yeye ndiyo mnenea wa muungano wa kisiasa wa Afrika ya Mashariki. Huwezi kuwa mnenea na mhujumu wa kanuni za msingi za muungano huo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: