Uncategorized

Misaada kwa wakimbizi Uganda yasimamishwa kutokana na ufisadi


Robert Matovu


Ufisadi Uganda umekithiri. Ukiona nchi inatumia maafa ya watu kama mtaji, jua kuna ukosefu mkubwa wa maadili. Baada ya Japan na Uingereza, Ujerumani imekuwa nchi ya tatu kukata mrija wa misaada ya fedha kwa ajili ya wakimbizi Uganda kutokana na kuzitafuna pesa wanazopewa.


Viongozi wa serikali ya Yoweri Museveni, wananufaika sana na kuwa na wakimbizi kitu ambacho wanakiona kama mradi wenye faida kubwa. Pamoja na manufaa ya kifedha kutokana na wakimbizi, utawala wake umegeuza ukimbizi kama mkondo wa kuyumbisha usalama wa nchi majirani hasa Rwanda na Sudan ya Kusini.


Baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wamekuwa wakifuja au kuiba misaada ya wakimbizi kwa kushirikiana na maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu. Mwandishi mahili na gwiji wa Uganda, Onyango Obbo, kupitia ujumbe wa twitter alisema Uganda imegushi idadi ya wakimbizi kwa zaidi ya laki tatu (300,000) kitu ambacho kiliwawezesha walaji kupata fedha za bure, na za kuwahujume majirani.


Kwa muda mrefu hakukuwa na mfadhiri aliyekuwa anaiomba serikali kuwajibika. Kuombwa uwajibikaji kumewayumbisha sana. Kugushi idadi ya wakimbizi nchini humo, siyo tatizo pekee. Hilary Onek, ni Waziri wa Uganda wa maswala ya Maafa na wakimbizi.


Hivi majuzi Waziri Onek alikaririwa akisema Uganda ni nchi yenye fadhila sana na ambayo imewapokea na kuwasaidia wakimbizi. Kukatwa kwa misaada kwa wakimbizi kumewaumbua, na kuionyesha dunia kuwa fadhila aliyoisema ni uongo tu, na mojawapo ya uozo wa miaka 33 wa utawala wa Museveni.


Mwaka jana, Umoja wa mataifa ulifanya upelelezi wa kina Uganda, na ukagundua ufisadi wa mamilioni ya dola za kimarekani zilizotolewa kuwasaidia wakimbizi. Kuwa na wakimbizi hewa zaidi ya 300,000, ni ishara ya uozo wa kimfumo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: