Uncategorized

Mkutano wa Kilele Utafanyika Angola Wakati Uganda Inashtakiwa Arusha

Robert Matovu


Jumatano tarehe 21 Agosti 2019, Luanda, Angola, kutafanyika mkutano wa kilele wa Marais nchini wa nchi nne za Angola, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.


Mkutano huu utapokea na kujadili mapendekezo ya serikali ya Angola katika kutatua mgogoro uliopo kati ya Rwanda na Uganda. Marais watakaohudhuria mkutano huo chini ya uenyekiti wa mwenyeji wao Rais João Lourenço wa Angola ni Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paul Kagame wa Rwanda, na Yoweri Museveni wa Uganda.


Mkutano unaotarajiwa, ni matokeo mkutano kama huo wa viongozi hao wa ukanda uliofanyika wa tarehe 12 Julai 2019, jijini Angola. Katika mkutano huo mwezi jana, Rais wa Angola alijitolea kuwa msuluhishi baada ya malalamiko ya Rwanda.


Uganda inashutumiwa kuwaunga mkono waasi na magaidi wanaoyumbisha usalama wa Rwanda. Na hili lilithibitishwa na jopo la wataalamu la Umoja wa Mataifa Disemba mwaka jana.
Wataalamu hawa walibaini kuwa Uganda ndiyo kitovu cha makundi ya RNC na FDLR kutafuta makurutu na mafunzo. Makundi haya ni wanachama wa muungano unaojiita ‘P5’.


Tatizo lingine kubwa linalolalamikiwa na Rwanda ni kuwateka, kuwatesa, kuwafunga kiholela na hata kuwapora mali zao.


Mamia na mamia wa raia wa Rwanda wamekuwa kwenye magereza ya Uganda kinyume cha sheria kiasi kwamba hakuna mtu aliye na hakika ni wangapi wanasota korokoroni kwa miaka kadhaa.


Tatizo hili limepelekea raia tisa wa Rwanda kuishitaki Uganda katika Mahakama ya Shirikisho la Afrika Mashariki (East African Court of Justice). Madai yao wanaitaka serikali ya Uganda iwalipe fidia Uganda kutokana na mateso, kukamatwa na kufungwa kiholela.
Tisa hao wanawakilishwa na mwanasheria Richard Mugisha wa Trust Law Chambers

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: