Uncategorized

Kuna mashaka Uganda itayatekeleza makubaliano na Rwanda

Robert Matovu


Mshikamano wa kikanda ni muhimu katika mahusiano ya nchi za Kiafrika. Mshikamano huo umeanza kuzaa matunda. Swala la msingi ni kupevuka na kufurahiwa kwa matunda hayo.


Tarehe 21 Agosti, jijini Luanda-Angola Rwanda na Uganda walitia saini aridhilihali au mkataba wa makubaliano ya kuboresha au kurejesha uhusiano wa nchi hizi mbili ambao umeyumba kwa zaidi ya miaka 20, na kudorora kwa zaidi ya miaka miwili sasa.


Rais Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda walisaini mkataba huo wa makubaliano mbele ya wapatanishi, Marais João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na shahidi wao Rais Sassou Nguesso wa Kongo-Brazzaville.


Ni makubaliano, ambayo yakitekelezwa yatapelekea kuwepo na utengamano wa mahusiano kati ya nchi hizi ndugu. Pia, makubaliano haya yalionyesha kuzingatiwa kwa mashtaka au malalamiko ya Rwanda.
Katika baadhi ya ibara za makubaliano hayo, zinazitaka pande mbili zilizokubaliana, kujiepusha na vitendo vya kuyahifadhi na kuyafadhili makundi yenye mipango bayana ya kuzihujumu nchi zao.


Uganda haijawahi kuishitaki au kuituhumu Rwanda kuwa inayahifadhi na kuyafadhili makundi yoyote yanayoipiga vita nchi hiyo. Pia Uganda haijawahi kuishutumu Rwanda kuwakamata kiholela, kuwatesa na kuwafunga kinyume cha sheria wananchi wake wanaoitembelea.
Aidha, kwa kutumia ushahidi wa kuaminika, kwa muda mrefu Rwanda inaishutumu Uganda kuwahifadhi na kuwafadhili makundi ya Rwanda National Congress (RNC) ambalo ni kundi la kigaidi na Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), ambalo kundi linaloongozwa na watu wanaoshutumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari.


Kuna mamia ya wanyarwanda ambao wanasota kwenye mahabusu yasiyofahamika kisheria nchini Uganda. Kati ya hao hakuna hata mmoja ambaye amefikishwa mahakani kwa mujibu wa sheria kama katiba ya nchi hiyo inavyoainisha. Wengi wao waliteswa kiasi cha kutosha kiasi kwamba serikali ya Uganda haiwezi kuwaachia kwa kuogopa kuumbuka.
Uganda imekuwa ikiihujumu Rwanda kiuchumi. Mifano ni ile ya kuzuia mradi wa kujenga reli (Standard Gauge Railway) ya kuiunganisha Rwanda na Kenya kupitia Uganda, kukataa nyaya za umeme kutoka Ethiopia kupita Uganda kwenda Rwanda na usafiri wa maziwa na madini kwenda Kenya na nchi nyingine.


Ishara mbaya
Rais Museveni akiwa angani kuelekea Luanda kwenye mkutano wa kilele, serikali yake iliamua kuyafungia magazeti ya Rwanda yanayosomwa kwenye mtandao. Kitendo hiki kiliwafanya wachunguzi wa mambo ya kisiasa kushuku kuwa Uganda haikuwa tayari kuyaheshimu makubaliano ya kurejesha utengamano wa mahusiano na Rwanda.
Kwa muda mrefu, wananchi wa Uganda, ukiacha watu wanaofuatilia kwa karibu yanayotokea, magazeti mengi ya Uganda yanaonekana kuyafumbia macho yanayotokea nchini mwao na kuwaacha wasomaji katika lindi la giza.


Baada tu ya kutiwa saini kwa mkataba wa Agosti 21, magazeti ya Uganda yalisusa kuchapisha maudhui ya mkataba. Na hilo lina uhusiano na kuyafungia magazeti ya Rwanda ya mtandaoni. Sababu kubwa, kama alivyobainisha mdadisi wa mambo ya kisiasa wa eneo hili, serikali ya Museveni haikutaka wananchi wake wajue ni nini kilichotokea Luanda. Hilo lingesababisha serikali yao kuumbuka kwa kuwa mkataba unaonyesha wazi kuwa Uganda iliikosea Rwanda.


Wanasiasa na vyombo vya habari vilianza kuzungumzia kufunguliwa kwa mpaka kati ya nchi hizi mbili kana kwamba ndilo tatizo lilisababisha kuwepo kwa mgogoro kati ya nchi hizi mbili. Waliwafanya wananchi waanze kufikiri kuwa biashara itaendelea kama kawaida. Hakuna hata mmoja kati yao, ambaye anazungumzia mamia ya Wanyarwanda wanaoteseka kwenye mahabusu bubu ya majasusi wa kijeshi la Uganda.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: