Uncategorized

Masoko ya Watumwa kwenye Magereza na Vituo vya Polisi Uganda

Robert Matovu


Wananchi wa Rwanda na Uganda wanasubiri serikali ya Uganda kupiga hatua za kuboresha uhusiano wa nchi hizi ndugu kama ilivyoainishwa na mkataba wa makubaliano wa Luanda yaliyotiwa sahihi tarehe 21 Agosti mwaka huu.


Hakuna dalili za kurejea kwa hali ya uhusiano wa kawaida. Mpaka sasa tume iliyotajwa katika makubaliano hayo haijaundwa. Wajumbe wa Kamati hiyo ni Mawaziri wa Nchi za Nje na wa Utawala wa Nchi hizo mbili. Katika tume hiyo pia, watawajumuishwa wakuu wao wa Upelelezi.
Mpaka hivi, sasa hadidu za rejea za tume hii hazijafahamika. Kuna mengi ya kuzungumzia na kutatua, yakiwemo wananchi wa Rwanda kwa mamia wanaoendelea kuteseka kwenye mahabusu na gereza zisizofahamika nchini Uganda.


Tume hii itawajibika kujadili kwa undani chanzo cha mfarakano na hasa malalamiko ya Rwanda dhidi ya Uganda ambayo yana zaidi ya miaka 20. Japo, mengi yamezungumzwa kuanzia mwaka 2017.
Kama kuna kuna tatizo linalopashwa kupewa kipaumbele katika majadiliano, ni wanyarwanda wanaofanyishwa kazi za suluba mithiri ya utumwa. Wanaotuhumiwa ni uongozi wa Polisi na Magereza wa Uganda hasahasa katika eneo la Kisoro, Kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Manusura na mashahidi wa utumwa huu, ni Felicien Uwizeye mwenye umri wa miaka 51, Jacob Ndayambaje mwenye umri wa miaka 36, Jimmy Habimana mwenye umri wa miaka 27 na Emmanuel Twizerimana mwenye umri wa miaka 25. Manusura wote hawa ni wazaliwa na wakaazi wa Mkoa wa Kaskazini.


Kwa zaidi ya mwaka mmoja, wanne hawa, licha ya kufungwa mahabusu na jela kinyume cha sheria, wanadai kuishi kama watumwa kwenye gereza za Uganda. Wahanga hawa wanadai ni sehemu ndogo tu ya wenzao wanaoteseka kwenye gereza za nchi hiyo, zikiwemo zinazofahamika na zisizofahamika.


Mmoja wao, Emmanuel Twizerimana anadai kuwa wanyarwanda wangejua yanayoweza kuwafika huko Uganda, hakuna anayeweza kudiriki kwenda kwenye nchi hiyo ya jirani. Twizerimana aliliambia gazeti moja hapa Rwanda kuwa alikamatwa mwezi Agosti Kanama 2018 katika mkoa wa Kusini Magharibi wa Kisoro. Alikuwa na mazoea ya kwenda huko kwa matembezi na biashara, siku alipofika huko akakuta kuna operesheni ya kuwakamata Wanyarwanda.


Bia kujua walikuwa na kosa gani, yeye na wanyarwanda wenzie walihukumiwa kufungwa jela kwa muda wa mwaka mmoja kwa kile alichokiita uonevu uliokithiri.


Yaliyowafika yanasimuliwa na Twagirimana. Polisi au magereza nchini Uganda wanafanya makubaliano na raia, hasa wakulima wenye kazi zinazohitaji vibarua. Kwa kuwa wafungwa kutoka Rwanda hawana mtetezi, viongozi polisi au magereza wanawachukua kwenda kuwalimia au kung’oa visiki vya miti. Kama waliofanya kazi ni 10, mapolisi au walinzi wa magereza wanapewa shilingi elfu hamsini (USh 50,000/= ) kwa siku.
“Kila wakija kutafuta wafungwa wa kuwalimia au kung’oa visiki, Askari magereza au mapolisi wanawambia wana Wanyarwanda na ndio wenye nguvu. Mnapewa kazi ya kukata miti na kung’oa visiki, na kubeba miti au visiki hivyo kuvipeleka wanakotaka wateja wa polisi na magereza. Anayeshindwa kufanya hiyo kazi anapigwa fimbo nyingi sana”. Twizeyimana alilielezea gazeti moja la Rwanda.


Twizeyimana anasema magereza ya Kisoro yamekuwa kama masoko ya watumwa. “Mkulima anakuja na kumwomba mkuu wa Jela fulani amtafutie wafungwa wa kinyarwanda 15, analipa fedha kutokana na siku anazotaka kufanyiwa kazi hizo za suluba.” Gereza ya Ndorwa ni mfano mmoja alioutoa, na Twizeyimana anadai kuna wafungwa zaidi ya 500 ambao ni raia wa Rwanda. Na wote hao wanateseka jela kinyume cha sheria. Kama kuna jambo linalohitaji kipaumbele, ni hili la watu kufungwa na baadaye kugeuzwa watumwa.


Kama kuna wafungwa 500, na kati ya hao kuna 400 wanaoweza kufanya kazi hizo za kitumwa, viongozi wa gereza wanapata kipato haramu cha Ush.2,000,000/= kwa siku. Tatizo hili la utumwa linastahili kupewa umuhimu wa kimataifa na serikali na watu husika wawajibishwe.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: