Uncategorized

Tume ya kuratibu utekelezaji wa Mkataba wa Luanda kuanza Kigali


Robert Matovu


Makubaliano ya Luanda ya kurejesha uhusiano na ujirani mwema kati ya Rwanda na Uganda hayajatekelezwa kama ipasavyo hadi sasa. Hata hivyo, kuna matumaini japo finyu. Leo Jumatatu, Septemba 16, ujumbe wa Uganda utakuwa Rwanda kwa mazungumzo rasmi na serikali ya nchi hiyo.
Kama inavyoainishwa na makubaliano ya tarehe Agosti 21, utekelezaji wake utaratibiwa na tume yenye Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje na wa Tawala za Mikoa wa nchi hizi mbili na pia Wakuu wa Usalama wa Taifa.
Ujumbe wa Uganda Kigali, unaongozwa na Waziri Sam Kutesa ambaye ndiye mwanadiplomasia mkuu wa Uganda. Mawaziri wa Nchi za Nje wa Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanategemewa kuhudhuria mkutano huo muhimu.


Warudishwa kama mzigo
Katika mazingira ya kutatanisha, Septemba 12, siku nne tu kabla ya tume hiyo kukutana kwenye kikao cha kwanza, wanyarwanda 32 walirudishwa Rwanda kutoka Uganda. Kutokana na barua iliyotiwa sahihi na Byesigye Marcellino, ambaye ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji wa Maswala ya Kisheria na Ukaguzi, watu hao walikuwa kwenye mikono ya Idara ya Ujasusi wa Kijeshi wa Uganda (CMI).


Swali moja muhimu linalopashwa kuulizwa serikali ya Uganda ni nguvu na mamlaka ya CMI. Idara hii ya CMI imegeuka kama State Research Bureau (SRB) ya utawala wa Dikteta Idd Amin Dada. CMI kama SRB ni kila kitu. CMI imechukua madaraka mengi ya Polisi, Idara ya Magereza, Idara ya Uhamiaji na katika utendaji wake haijali Mahakama na taratibuu zote za kikatiba za kulinda Haki za Binadamu.


Mfano mmoja dhahiri ni hawa wanyarwanda 32 waliorejeshwa. Katika barua ya kuwarudisha Rwanda, idara ya Uhamiaji ya Uganda, inajipambanua na kusema kuwa watu hao walikuwa katika mikono ya CMI. Lakini kama inavyotajwa, watu hao wanadaiwa walikamatwa kwa kuwa hawakuwa nchini humo kihalali.


Kwa kawaida, katika nchi zote duniani, swala la uhamiaji, halali au haramu, linavihusu vyombo vya ulinzi hususan Polisi, na hasahasa Idara ya Uhamiaji na Mahakama. Watu wakikamatwa kwa shutuma za kuwa kwenye nchi nyingine kinyume cha sheria, Idara ya Uhamiaji inaiomba Mahakama kuwarejesha makwao kwa mujibu wa sheria.


Kama ni raia wa Rwanda wamekamatwa, mara nyingi kwa kuchongewa na magaidi wa Rwanda National Congress (RNC) basi CMI inachukua madaraka yote ya kuwashughulikia. CMI watahakikisha mtu atakamatwa ateswe, akataliwe haki ya utetezi na akifa wana hakika hawaulizwi.


Haya ndiyo yanawasibu raia wa Rwanda wanaokamatwa, kuteswa, kuporwa mali zao na wenye bahati hutupwa mpakani kama mzigo usio na mwenyewe.


Kama kuna hoja zinazopashwa kupewa umuhimu na kipaumbele katika mazungumzo yanayoanza leo kati ya ujumbe wa Rwanda na Uganda ni hili la Raia wa Rwanda kunyanyaswa na CMI na pili, ni hili la baadhi ya Viongozi wa Uganda kuwasaidia kwa hali na mali.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: