Uncategorized

Mauti baada ya mateso dhidi ya raia wa Rwanda

Robert Matovu


Licha ya kukutana jijini Kigali kwa tume ya kuratibu makubaliano ya Angola, hali ya utata inazidi kutanda. Mkutano huo ulioukutanisha ujumbe wa Uganda ukiongozwa na Waziri Sam Kutesa wa Mambo ya Nchi za Nje, na wa wenyeji wao wa Rwanda ukiongozwa na Waziri wa Nchi wa maswala ya Afrika Mashariki, Olivier Nduhungirehe.


Vipengele muhimu katika mazungumzo hayo vilikuwa ni kuachiliwa kwa raia wa Rwanda walio kwenye mahabusu na magereza ya Uganda kinyume cha sheria, na Uganda kuacha kuvipa msaada vikundi vya Rwanda National Congress (RNC) na FDLR vinavyoipinga serikali ya Rwanda.


Tarehe 17 Septemba, 2019, siku moja tu baada ya mkutano huo na tangazo la pamoja lililoorodhesha vipavipaumbele kukiwemo kuachiliwa kwa wanaoteseka magerezani, vikwazo vilianza kujitokeza kwenye upande wa Uganda.


Gazeti la kwenye mtandao ‘Command Post’ linaloendeshwa na Idara ya Ujasusi wa Jeshi la Nchi hiyo (CMI) lilichapisha Makala yenye kichwa cha habari kisemacho “Uganda haipashwi kumuachia huru muuaji Rene Rutagungira.” Katika Makala hayo wakaorodhesha sababu zao kadhaa kuthibitisha ni kwa nini Rutagungira abaki jela, zaidi ya miaka miwili baada ya kukamatwa bila ya kufikishwa mahakamani.


Idara hii ya CMI ninayoilinganisha na State Research Bureau (SRB) chini ya Dikteta Idd Amin, haiwajibiki kwa mhimili wowote wa dola kukiwemo mahakama na Bunge. Mtu pekee anayeweza kuwakanya na kuwapa mwongozo CMI ni Rais Yoweri Kaguta Museveni, mdogo wake Jemadari Salim Saleh au Luteni Jemadari Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mwanae Rais Mjuseveni.


Tamko la CMI la ni nani aachiliwe na ni nani asiachiliwe, inaonekana siyo la kujadiriwa na Wizara ya Mambo ya nchi za nje ya Uganda, au vyombo vya Mahakama na Polisi vya nchi hiyo. CMI hufanya ilitakalo, chini ya uongozi wa Brigedia Jemadari Abel Kandiho.


Ukiacha raia wa Rwanda, na wengine wa Uganda wanaofungiwa kwenye sehemu zinazofahamika, watu wengi hufungiwa kwenye jela ndodo ndogo za siri zijulikanazo kwa kiingereza kama “safe house” pamoja na kwamba hakuna usalama katika nyumba hizo.


Rutagungira alinyakuliwa na makachero wa CMI mwezi Agosti 2017, licha ya familia yake na wakili wake kuomba afikishwe mbele ya mahakama kujibu shutuma dhidi yake, ombi hilo halikutekelezwa.


Baada ya kukamatwa kwa Rutagungira, serikali ya Uganda ilikana hajakamatwa. Serikali ilikiri kukamatwa kwake baada ya kuonyeshwa video za CCTV kama ushahidi. Picha hizi ziliwaumbua makachero wanaofahamika kuwa ni watumishi wa CMI, kitu ambacho serikali isingeweza kukikana.


Mwanzoni alishutumiwa kufanya mauaji, baadaye CMI ikadai alikamatwa na silaha alizokuwa nazo kinyume cha sheria. Baada ya mashtaka hayo kudhihirika hayana mashiko, wakazua kuwa Rutangungira alihusika kwenye operation ya kumrejesha Rwanda Luteni Joel Mutabazi aliyekuwa na kesi ya uhaini Rwanda.


Kurejeshwa kwa Lt. Mutabazi kulitokana na maafikiano ya Serikali za Rwanda na Uganda kubadilishana wahalifu. Wakati wa kurejeshwa kwa baadhi ya watuhumiwa akiwemo Lt. Mutabazi na wengine wanane (jumla 9), namba ndogo ukilinganisha na watuhumiwa wa uhalifu 26 waliorudishwa Uganda kutoka Rwanda.


Na shutuma hizo dhidi ya Rutagungira, zilimhusisha aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Jemadari Kale Kayihura. Hata hivyo, kutokana na gazeti la mtandao la ‘Virunga Post’ aliyeruhusu kurejeshwa kwa Lt. Mutabazi siyo Gen. Kayihura aliyekuwa nje ya nchi, bali Jemadari Muhoozi Kainerugaba.
Kesi ya Rutagungira siyo ya kipekee, kwani inajulikana kwamba kwenye gereza na “safe houses” za Uganda, kuna raia wa Rwanda zaidi ya 280, angalau. Kati ya hao ni Augustin Rutayisire na Emmanuel Rwamucyo waliokamatwa na kuporwa fedha zao mwezi Mei 2018, na baadae kusingiziwa kosa la kuwa na silaha ndani ya gari lao.
Mateso na Vifo
Raia wa Rwanda kwa jina la Hategekimana Silas alikutwa na mauti kutokana na mateso aliyoyapata katika gereza za Uganda. Marehemu Hategekimana alikamatwa na kufungiwa Uganda tarehe 25 Mei, 2019. Baada ya mateso makali, tarehe 12 Juni, 2019 alitupwa kwenye mpaka wa Kagitumba akarudishwa Rwanda. Hategekimana aliaga dunia tarehe 31 Agosti akiwa na umri wa miaka 43.


Uchunguzi wa kitaalam uliofanywa baada ya kifo hicho, ulithibitisha kuwa mateso aliyoyapata yalikuwa ni chanzo cha kifo hicho cha Hategekimana. Huyu siyo mhanga pekee wa mateso haya ya CMI. Johnson Nunu alikuwa mfanyabiashara aliyekuwa na makazi Ntungamo Uganda. Alinyakuliwa na CMI tarehe 19 Desemba, 2017 kutoka nyumbani kwake. Serikali ya Rwanda imeiomba Uganda kufanya uchuguzi wa kina kuhusu kifo hiki.
Kwa muda mrefu alifungwa na kuteswa kwenye kambi ya kijeshi ya Mbuya jijini Kampala. Mateso aliyoyapata akiwa jela na kusababisha kujeruhi ini lake, ukiongeze na kumnyima matibabu ya kisukari, siku chache baada ya kuachiwa alifariki dunia. Mauti yalimkuta Johnson Nunu tarehe 17 Agosti mwaka huu.


Hakuna aliye na uhakika kuwa haki itatendeka kwa familia za marehemu waliokufa kutokana na mateso na kutelekezwa na serikali ya Uganda. Vile vile hakuna ishara kuwa msaada kwa vikundi vya RNC na FDLR utasitishwa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: