Uncategorized

Katika 25 wanaoshitakiwa uhaini Rwanda kuna raia wa Burundi na Uganda

Robert Matovu
Baada ya Jeshi la Kongo kuwapiga na kuwafurukusha magaidi wa Rwanda National Congress (RNC), baadhi yao walikamatwa mateka wakakabidhiwa kwa serikali yqa Rwanda. Kati ya hao mateka ni aliyekuwa Kamanda wa Operesheni za kijeshi wa RNC. Habari za kukamatwa kwao zilitangazwa na Jeshi la Kongo tarehe 28 Juni 2019.


Tarehe 2 Oktoba, 25 ya hao waliokamatwa na kurejeshwa Rwanda walifikishwa mbere ya Mahakama ya Kijeshi Daraja la kwanza yaliyoko katika kitongoji cha Nyamirambo jijini Kigali.
Wote wanashitakiwa makosa ya jinai na uhaini kukiwemo kuunda kundi la kijeshi haramu; kutaka kuupindua utawala halali wa nchi; na kushirikiana na nchi za nje katika mipango ya kuipiga vita Rwanda.
Kati ya hao, wa kwanza ni Meja (Mstaafu) Habibu Mudathiru. Huyu Mudathiru alikuwa na cheo cha Kanali katika RNC na akiwa Kamanda mkuu wa kijeshi kwenye misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Uganda na Burundi kuna maswali
Kati ya hawa 25 waliofikishwa mahakamani, kuna wanyarwanda waliokuwa wakiishi kama wakimbizi Uganda, lakini pia kuna Warundi na Waganda kati yao.
Wenye asili ya Rwanda ni Vedaste Ngendakumana (mwenye umri wa miaka 32); Rugamba Viateur Hagenimana (mwenye umri wa miaka 27); Assier Mfitumukiza (mwenye umri wa miaka 29); Patrick Twizerimana (mwenye umri wa miaka 29) na Diogène Bihoyiki (mwenye umri wa miaka 37).
Wengine ni Claude Haguma (mwenye umri wa miaka 23); Ildephonse Mbarushimana (mwenye umri wa miaka 22); Innocent Habanabakize (mwenye umri wa miaka 26); Andre Gashumba (mwenye umri wa miaka 53); Shadrac Ngiruwera (mwenye umri wa miaka 23) na Habarurema Jackson (mwenye umri wa miaka 25)
Raia wa Uganda ni Suleimani Rugambwa (mwenye umri wa miaka 43) mzaliwa wa Masaka; Joseph Gakwerere (mwenye umri wa miaka 18) ambaye hakueleza kwao asili ni wapi na Desiderion Fred (mwenye umri wa miaka 23) mwenyeji wa Rubenge wilaya ya Mubende.
Raia wa Burundi ni Jean Bosco Havyarimana (mwenye umri wa miaka 30); John Minani (mwenye umri wa miaka 37) ambaye anadai kwao ni Mkoa wa Kayanza. Jean Marie Nsabimana (mwenye umri wa miaka 28) ambaye kwao ni mkoa wa Cibitoke; Leverien Yukamazina (mwenye umri wa miaka 22) kutoka mkoa wa Muramvya; Yisa Ndikurugendo (mwenye umri wa miaka 30) mwenyeji wa Bujumbura; Ildephonse Rusigariye (mwenye umri wa miaka 23) alizaliwa Rwanda lakini sasa hivi alikuwa anaishi Burundi na Yisa Ndikumana na Jean de Dieu Ndirahira (mwenye umri wa miaka 32) ni mwenyeji wa mkoa wa Cibitoke.
Kati ya hao waliokamatwa na kufikishwa mahakamani ni Lambert Ndibanje mwenye umri wa miaka 23, ana asili ya Burundi, uraia wa Malawi lakini na kabla ya kwenda kwenye Misitu ya Kongo alikuwa anakaa Rukore.
Waendeshamashitaka Major Ruyonza na Capt Rugambwa waliiambia mahakama jinsi washitakiwa walivyojiunga na kundi hili la RNC kwenye eneo la Minembwe lililoko Jimbo la Kivu ya Kusini nchi DRC. Wote walihamasishwa na kujiunga na kundi hilo wakisaidiwa na Idara ya Ujasusi wa Kijenshi wa Uganda/Chieftancy of Military Inteligency (CMI) hususani huyu Major Mudathiru na mwenzie KApteni Sibo (aliuawa na Jeshi la Kongo) shuguri zao Uganda zilikuwa zinaratibiwa na Capt. Johnson (hawakutaja jina linguine) wa UPDF.
Wanaowasaidia RNC
Operesheni za RNC nchini Burundi zinaratibiwa na Kanali Ignace Sibomana ambaye ni Mkuu wa wa idara ya Ujasusi wa Kijeshi (J2) nchini humo, akisaidiwa na Meja aliyetajwa kwa jina moja la Bertin.
Aliyetajwa katika uratibu wa operesheni za RNC nchini Uganda ni Richard Mateeka, ambaye ana wajibu wa kuvisaidia vikundi vilivyo chini ya mwavuli wa P5 kukiwemo kutoa mafunzo na silaha. Baada ya kupata mafunzo na silaha wanapelekwa kwenye maeneo kadhaa ya DRC kuwafunza wengine. Mafunzo hayo yanafanyika katika maeneo ya Bijabo, Minembwe na Masisi kwenye majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini.
Kundi hili la RNC linaloongozwa na Kayumba Nyamwasa. Huyu Kayumba anaishi Afrika ya Kusini lakini shubguli zake nyingi zinazohusu mipango ya kuihujumu Rwanda zinafanyika Uganda na Burundi kama ilivyowahi kutajwa katika Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2018.
Kesi hii inatalajiwa kufuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kutokana na uzito wa ushahidi utakaotolewa na upande wa mashitaka na watuhumiwa wakati wa utetezi.
Operesheni za Kijeshi za DRC ni utekelezaji wa makubaliano ya marais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paul Kagame wa Rwanda na João Lourenço wa Angola wa kuvifyeka vikundi vya kijeshi vinavyovuruga usalama katika nchi hizi hususan DRC.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: