Uncategorized

Makamishna wa Rwanda National Congress Uganda

Robert Matovu
Kuna nini Kampala? Ni swali linaloulizwa na wadadisi wa mambo ya kisiasa hasa kwenye miji mikuu ya Uganda, Rwanda, Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Tarehe 16 Septemba mwaka huu, wajumbe wa Serikali za Rwanda na Uganda walikutana kwa mazungumzo mjini Kigali katika mkutano wa kwanza wa kutekeleza makubaliano ya Luanda ya tarehe 21 Agosti.
Wajumbe wa nchi hizo mbili waliongozwa na Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Rwanda na Uganda. Katika mkutano huo, baadhi ya waliyokubaliana ni kukutana nchini Uganda baada ya siku thelathini (30) kutathimini utekelezaji wa maswala yaliyoafikiwa. Kati ya yaliyotakiwa kutekelezwa ni pamoja na kuwaachia raia wa Rwanda wanaoteseka kwenye magereza na mahabusu haramu nchini Uganda.


Kama siku 30 zingeheshimiwa, mkutano huo ulipashwa kufanyika tarehe 16 Oktoba nchini Uganda. Siku hiyo iliwadia bila lolote kusemwa na serikali ya Uganda. Siku tano baada ya muda huo kuisha, swali ni asili ya huo ukimya.


Gazeti moja la mtandao nchini lijulikanalo kama ‘Chimpreports’ likinukuu Wizara yao ya Mambo ya Nchi za Nje limetangaza ilituma Kigali ukaribisho wa mkutano unaopashwa kufanyika tarehe 13 Novemba.
Waziri wa Nchi wa Rwanda wa maswala ya Afrika Mashariki, Olivier Nduhungirehe, amekunasha kuwepo kwa barua hiyo. Wakati huo huo Rais Yoweri Museveni hakuthibitisha au kukanusha yaliyotajwa na Chimpreports, gazeti lijulikanalo kuwa ni chombo cha CMI. Ulaghai huo ni kitu cha kawaida kwa Rais Museveni
Wafungwa na Mateso
Siyo utabiri, ila ni ukweli tu kuwa kimya kinasababishwa na kutotekelezwa kwa yale yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa Kigali wa mwezi jana. Mamia ya wanyarwanda wanazidi kusota magerezani kinyume cha sheria, baadhi yao wakiwa katika hali hiyo kwa zaid ya miaka miwili.


Tarehe 18 Oktoba, mawakili wanaojihusisha na maswala ya Haki za Binadamu nchini Uganda walibainisha kuwa kuna zaidi ya Wanyarwanda mia moja (100) wanaoishi kwa mateso makubwa katika mahabusu ya Idara ya Ujasusi wa Jeshi la Uganda (CMI).


Hayo yalisemwa na mawakili wa ‘Kiiza & Mugisha and Company Advocates’ kwenye mkutanoo na wana wa Habari uliofanyika Jijini Kampala katika Speke Hotel. Katika mkutano huo mawakili waliitaka serikali ya Uganda na hususani CMI kuwaachia Raia hao wa Rwanda au wafikishwe kwenye mahakama ya kiraia nchini humo.


Mmoja wa mawakili hao, Anthony Odur, alinukuliwa akisema Waganda, Wanyarwanda na Wakongomani hawana tofauti. Haki zao zinastahili kuheshimiwa. Tutazidi kuwawakilisha kama watetezi. Kila siku wanateswa na sisi kama wawakilishi wao na familia zao tumeshindwa kuwafikia. Katiba inapaswa kuheshimiwa.” Alisema ni jambo la aibu kuwa serikali ya Uganda haiwezi kuwaachia raia hawa wa Rwanda wanaoishi kwa mateso. Alitoa wito kwa serikali kuwaachia bila masharti yoyote.
Wengi wao wamekuwa jela tangu mwaka 2017. Kati ya hao, Wakili Oduor aliwatajamahabusu Rene Rutagungira, Irakaremye Claude, Rwamucyo Emmanuel na Rutayisire Augustine walionyimwa mdhamana baada ya kufikishwa kwenye Mahakama kuu ya Kijeshi. Wakili Kiiza alisema hakuna sababu yoyote kisheria inayowafanya wateja wake wafikishwe kwenye Mahakama ya Kijeshi wakati wao ni raia. Kwa maoni yake kesi zao ni wajibu wa polisi na siyo CMI.


Kiongozi wa RNC Uganda
Katika makubaliano ya Uganda na Rwanda ya tarehe 16 Septemba, ni Uganda kusitisha ufadhili wa makundi yanayoanda vita dhidi ya Rwanda. Katika makundi hayo ni lile la Rwanda National Congress (RNC).
Benjamin alias Ben Rutabana ni Kamishina wa Kukuza Uwezo yuko nchini Uganda tangu tarehe 5 Septemba 2019. Hili lilithibitiswa na barua ya familia ya Rutabana ya tarehe 2 Oktoba 2019 wakidai wamekosa mawasiliano naye.


Barua hiyo inathibitisha kuwa Ben Rutabana alikutana na Frank Ntwari ambaye ni Kamishna wa RNC anayejihusisha na kuhamasisha vijana. Kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe, Ben Rutabana alipokelewa na Kanali (mstaafu) Kaka Bagyenda ambaye ni Mkuu wa idara ya Usalama wa Ndani /Internal Security Organisation (ISO) wa Uganda.


Kupokelewa kwake kama mtu muhimu, kulizidi kudhihilika pale alipopewa Luteni Jack Erasmus Nsangiranabo kama mpambe na mkuu wake wa itifaki. Kutokana na gazeti moja la Rwanda linalofuatilia kwa karibu yanayotokea Uganda Rutabana yuko Uganda kufanya ukaguzi wa mafunzo wanayopewa makurutu wa RNC.


Rutabana au Ntwari siyo viongozi pekee wa RNC wanaoendesha shughuli zao nchini humo. Charlotte Mukankusi ambaye ni mkuu wa diplomasia wa RNC, alikuwa Uganda mwanzoni mwa mwaka huu na anatumia pasipoti ya Uganda.


Rais Museveni alithibitisha kuonana na Charlotte, Eugene Gasana na Tribert Rujugiro ambao ni viongozi wa RNC

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: