Uncategorized

Hatimaye Uganda Yataja Tarehe ya Mazungumzo na Rwanda

Na: Robert Matovu
Baada ya muda bila kujua ni lini mkutano wa usuluhishi wa mzozo kati ya nchi yetu ya Uganda na Rwanda, inawezekana ukafanyika tarehe 13 Novemba 2019. Hayo yamethibitishwa na Waziri wa Nchi wa Rwanda wa maswala ya Afrika ya Mashariki, Olivier Nduhungirehe.
Waziri Nduhungirehe amelieleza gazeti la mtandao Rwanda, Igihe kuwa wamepata mwaliko kutoka Uganda ulioainisha mkutano utafanyika siku nane zijazo.


Mchakato wa usuluhishi ulipangwa kwenye mkataba wa makubaliano ya kurejesha uhusiano mwema kati ya Rwanda na Uganda wa tarehe 21 Agosti. Ulitiwa sahihi na Maraisi Paul Kagame na Yoweri Kaguta Museveni jijini Luanda, Angola wakiwepo wasuluhishi ambao ni Marais João Lourenço wa Angola, Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na shahidi wao Rais Sassou Nguesso wa Kongo-Brazzaville.
Mkataba huo ulikuwa na vipengele, takribani vyote, vilivyozingatia malalamiko ya Rwanda dhidi ya Uganda, kitu kilichosababisha Uganda kuyafungia magazeti mengi ya Rwanda yanayochapishwa kwenye mtandao. (tazama zaidi)


Mkutano huu wa kusuluhisha mgogoro wa zaidi ya miaka miwili, umecheleweshwa na Uganda kwa karibu mwezi mzima kwa sababu ulipashwa kufanyika tarehe 16 Oktoba.
Malalamiko ya Rwanda, na ambayo siyo rahisi kuyakana ni matatu: Kwanza ni lile la kuihujumu Rwanda kibiashara na kiuchumi. Mfano ni lile la kuyazuia au kuyachelewewesha magari ya mizigo ya Rwanda yanayosafirisha mizigo kwenda Kenya kupitia Uganda.
Lalamiko la pili la Rwanda ni lile la Uganda kuwahifadhi na kuwasaidia makundi ya kigaidi yanayopanga kuishambulia Rwanda. Makundi hayo ni lile la Rwanda National Congress (RNC) na lile la FDLR lenye itikakadi ya mauaji ya kimbari na lenye viongozi waliofanya mauaji hayo dhidi ya watutsi mwaka 1994.


Tatizo lingine kubwa ni kuwakamata, kuwafunga kinyume cha sheria, kuwatesa na kuwapora mali raia wa Rwanda wakiwa Uganda. Na yote haya hufanywa na idara ya ujasusi wa kijeshi wa Uganda CMI kwa kifupi. Hakuna raia hata mmoja wa Rwanda ambaye amewahi kufikishwa mahakamani nchini Uganda licha ya tuhuma zisizo na mashiko. Wengi waho hukamatwa bila mashitaka na baadae huitwa majasusi.
Katika mkutano wa usuluhishi uliofanyika Kigali tarehe 16 Septemba, serikali ya Uganda ilikabidhiwa orodha ya majina zaidi ya mia moja ya Raia wa Rwanda ambao walikamatwa na kufungwa kikatili. Kuna fununu kuwa, hivi karibuni, kuna baadhi ya hao mahabusu waliohamishwa kutoka mahabusu ya CMI na kuhamishiwa kwenye vituo tofauti vya Polisi.
Serikali ya Uganda haijatoa tamko lolote kuhusu wanyarwanda hao wanaosota kwenye jela za Uganda baadhi yao wakifanyishwa kazi za utumwa. (tazama zaidi)


Katika mkutano wa Kigali wa mwezi uliopita, wajumbe wa Rwanda-Uganda walikuwa na mapendekezo kadhaa yaliyokuwa ya manufaa, na ambayo yangeweza kuwa chanzo cha kuejesha mahusiano mazuri. Utashi wa kisiasa wa Uganda ulikuwa ni muhimu kwa sababu mengi yaliyovuruga au kukwamisha uhusiano wa nchi hizi mbili unatoka Kampala na siyo Kigali. Walikubaliana kuwa iwapo kuna raia wa nchi moja atakamatwa na nyingine akishukiwa kuvunja sheria, basi mkondo wa sheria ufuatwe. Walikubaliana pia kuepuka propaganda za kuhujumiana katika magazeti na mitandao ya kijamii; kuacha vitendo vya kuhujumu usalama wa majirani (Uganda ikiwa ni mshukiwa mkuu) na kuwepo kwa mkataba wa kubadilishana wahalifu.


Ujumbe wa Rwanda uliongozwa na Balozi Olivier Nduhungirehe, ambaye ni Waziri wa Nchi wa maswala ya Afrika Mashariki, ule wa Uganda ukiongozwa na Sam Kutesa ambaye ni Waziri wa mambo ya Nchi za Nje. Katika ufunguzi wa mkutano huo wa kwanza kufuatia makubaliano ya Luanda, kwa niaba ya wasuluhishi, alikuwepo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Angola, Manuel Domingos Augusto, na Gilbert Kankonde Malamba, ambaye ni Naibu Waziri Mkuu wa DRC anayehusika na Mambo ya ndani.


Aidha, ujumbe wa Uganda ulikuwa na Jemadari Jeje Odongo Abu, Waziri wa Mambo ya Ndani; Balozi Joseph Ocwet ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Nje; the Director-General External Security Organisation (ESO), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, William Byaruhanga na Balozi wa Uganda nchini Rwanda, Oliver Wonekha.
Wajumbe wa Rwanda walikuwa ni Johnston Busingye—Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu; Waziri wa Serikali za Mitaa—Prof. Anastase Shyaka; Balozi wa Rwanda nchini Uganda, Frank Mugambage; Joseph Nzabamwita—Mkuu wa Usalama wa Taifa na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Nje—Anaclet Kalibata.


Uzito wa Ujumbe wa pande mbili katika mkutano wa kwanza wa Kigali, ulikuwa ni wa matumaini. Swali ni yatakayozungumzwa na kutekelezwa baada ya Mkutano mtalajiwa wa Kampala!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: