Uncategorized

Kipigo cha waasi mashariki mwa Kongo ni majonzi kwa Rais Museveni

Na Robert Matovu


Mwaka wa 2019 ni mwaka utakaokumbukwa katika makundi yanayoipinga serikali ya Rwanda. Kwa makundi hayo, ya FDLR, RUD-Urunana, RNC na CNRD/FLN ni mwaka unaoisha kwa vilio na machozi. Wenye majonzi makubwa pi, ni baadhi ya viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Ugwnda akiwemo rais Yoweri Kaguta Museveni mwenyewe. Viongozi hao wa Uganda ni wafadhili wa makundi haya.
Kilio hicho kinatokana na uamuzi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokarasia ya Kongo (DRC) inayoongozwa na Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa kuyangoa makundi ambayo yamekuwa yakiitumia ardhi ya nchi hiyo kuwahujumu majirani.
Mwezi Desemba mwaka jana, maofisa wa ngazi ya juu sana wa kundi la FDLR walikamatwa na Jenshi la DRC wakitokea Uganda walipokuwa wamekaribishwa na serikali ya Rais Yoweri Kaguta Museveni ili waanzishe uhusiano wa karibu na kundi linguine la RNC la Kayumba Nyamwasa. Maofisa hao ni Ignace Nkaka alias La Forge Fils Bazeye ambaye alikuwa msemaji mkuu wa FDLR na Luteni Kanali Nsekanabo Jean Pierre alias “ABEGA” aliyekuwa mkuu wa idara ya Upelelezi wa kijeshi wa kundi hilo.
Baada ya kukamatwa maofisa hao wa ngazi ya juu walipelekwa Kinshasa na baadaye Rais Joseph Kabila akaamua kuwarejesha Rwanda. Ni dhahiri uamuzi huo ulimsononesha sana Rais Museveni na viongozi wa idara ya ujasusi wa jeshi la Uganda ambao fadhiri wa vikundi hivyo vinavyotwangwa.
Kurejeshwa Rwanda kwa Bazeye na Abega, kuliipa serikali ya Rwanda fursa ya kupata habari za kiintelijensia katika uhusiano wa kundi lao na Uganda. Isitoshe habari hizo za kiintelijensia zilitumiwa na Serikali ya DRC kuwasaka waasi hao na hatimaye kuuawa kwa kamanda mkuu wa FDLR, Luteni Jemadari Sylvestre Mudacumura na baadhi ya manaibu na wasaidizi wake.
Operesheni hizo, zilipelekea kupata habari nyingi zaidi za kiintelijensia na kupelekea kupigwa kijeshi hadi kuuawa na kukamatwa kwa wapiganaji na makamanda wa kundi la RNC. Kati ya hao waliokamatwa na jenshi la DRC ni Meja Habib Mudathiru.
Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17 Oktoba waasi 45 wapiganaji wa kundi la RUD-Urunana walishambulia kijiji kimoja katika wilaya ya Musanze Kaskazini mwa Rwanda. Katika shambulio hilo, waliwaua watu kadhaa kabla ya kuzidiwa nguvu na vyombo vya usalama vikiwemo Jeshi na Polisi. Wengi kati ya walioshambulia walikamatwa na wengineo kuuawa. Katika ya wale waliokamatwa, walikutwa na simu zilizobainisha kuwa walikuwa na mawasiliano ya uratibu kutoka kwa Philemon Mateke ambaye ni Waziri wa Maswala ya Ukanda.
Kukamatwa mateka kwa walioshambulia Rwanda, ilikuwa ni baraka kwa sababu habari za kiintelijensia walizozitoa, kulipelekea jenshi la DRC kuwashambulia waasi hawa na kumuua kamanda wa RUD-Urunana Brigedia Juvenal Musabyimana alias Jean Michel Africa.
Mashambulio haya ya RDC yameyasambaratisha makundi haya katika majimbo ya Kivu za kusini na Kaskazini mashariki mwa DRC. Jana tarehe 16 Desemba, DRC iliwarejesha wapiganaji 291 wa CNRD/FLN akiwemo Komanda wao Joseph Gatabazi, alias Gatos Avemaria, Anthère Ntamuhanga, wenye vyeo vya Luteni Kanali watatu (3) Meja watatu (3) na msemaji wao Kapteni Herman Nsengimana. Huyu msemaji wao alikuwa mpya baada ya msemaji wao Callixte Nsabimana kukamatwa na kurejeshwa Rwanda kutoka visiwa vya Ngazija (Comoro).
Kuzidi kupigwa kijeshi kwa makundi haya na walotekwa kurudishwa Rwanda, kunaongeza ushahidi wa uhusiano wa Uganda na Makundi haya.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: