Uncategorized

Wanyarwanda 7 Waachiwa na Mahakama Kuu ya Kijeshi Uganda: Ni Hatua Muhimu lakini haitoshi

Na Robert Matovu


Wakati mamia ya Raia wa Rwanda wakizidi kufungwa kuteswa na hata kuuawa nchini Uganda, leo hii Mahakama Kuu ya Kaijeshi nchini Uganda imewaachia huru mahabusu saba kati yao. Kati ya hao saba walioachiwa huru na mahakama hiyo chini ya uongozi wa Luteni Jemadari Andrew Gutti, ni Rene Rutagungira, Claude Iyakaremye, Emmanuel Rwamucyo na rafiki yake Augustine Rutayisire, Bahati Mugenga, Etienne Nsanzabahizi na Charles Byaruhanga.


Ikumbukwe kuwa huyu Rene Rutangungira amekuwa gerezani kama mahabusu, bila kufunguliwa mashtaka, tangu tarehe 7 Agosti 2017. Rutangungira alinyakuliwa na kikosi cha majasusi wa Idara ya Upelelezi wa Kijeshi nchini Uganda (CMI) kutoka karibu na anapoishi kwenye kitongoji cha Bakuli, Jijini Kampala.


Akitangaza uamuzi wa kuwaachia wafungwa hao katika Mahakama hiyo iliyopo Makindye, kwenye Mji Mkuu wa nchi hiyo, Lt.Gen. Gutti alibainisha kuwa upande wa mashtaka uliamua kufuta mashtaka baada ya kukosa ushahidi dhidi ya watuhumiwa.
Mawakili wao Eron Kiiza, Anthony Odur, Gawaya Tegulle na wengine waliokuwa hapo mahakamani, kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwa mashtaka yaliyokuwa yakitajwa na Idara hiyo ya upelelezi ni upuuzi mtupu.


Wakili Kiiza aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa hapo kuwa “Hakukuwa na chembe hata ndogo ya ushahidi dhidi ya wateja wetu”. Akasisitiza kuwa kilichofanywa na vyombo vilivyowakamata na kuwafunga na kuwatesa, ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na wa haki za binadamu.


Tukio hili la kuwaachia hawa saba, limethibitisha madai ya serikali ya Rwanda kuwa mamia ya wanyarwanda waliokuwa katika jela na mahabusu nchini Uganda ulikuwa ni wa unyanyasaji wa kikatili.
Kuachiwa huku kwa wafungwa saba kunafuatia hatua ya Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kumtuma mjumbe maalum kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda. Ujumbe huo wa kutaka kurejesha uhusiano mwema kati ya nchi hizi mbili alipewa Adonia Ayebare, ambaye ni Balozi wa Uganda kwenye Umoja wa Mataifa, New York.


Huyu Balozi Ayebare, ni ndugu wa damu wa Brigedia Jemadari Abel Kandiho ambaye ni mkuu wa CMI ambayo ni mtuhumiwa katika kuwakamata na kuwatesa wanyarwanda. Pia, CMI ndiyo mratibu mkuu wa serikali ya Uganda katika kufanikisha msaada unaopewa makundi ya FDLR na RNC.


Pamoja na kuwa Rais Museveni kuonyesha matumaini ya kurejea kwa uhusiano baada ya Ayebare kupokelewa Kigali na kufikisha ujumbe kwa Rais Kagame, asilimia ya wafungwa waliosalia magerezani na sehemu zisizo halali ni kubwa kiasi cha kurejesha imani ya ujirani mwema.
Matumaini pia yanaweza kurejeshwa iwapo Rais Museveni atawaachia wote waliofungwa kinyume cha sheria na kuacha kuyafadhiri wazi wazi makundi yanayoendesha hujuma dhidi ya Rwanda.


Kwa muda mrefu, kwa vielelezo na ushahidi, viongozi wa Rwanda wamekuwa wakiishutumu Uganda kuwa inafadhiri makundi ya kuihujumu Rwanda. Shutuma hizi unazikuta hata kwenye makubaliano ya Luanda ya tarehe 21 Agosti 2019.


Alipoulizwa kuhusu ujumbe wa Rais Museveni kupitia kwa mjumbe maalum Balozi Ayebare, Rais Kagame aliiambia Televisheni ya Shirika la Utangazaji Rwanda (RBA) kuwa kinachoweza kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizi mbili ni kuepukana na sababu au viini vya mgogoro uliopo. Kati ya hivyo vikwazo, ni kuwafunga raia wa Rwanda kiholela na kuyakumbatia makundi ya kigaidi kama FDLR, RNC na RUD-Urunana.


Wakati wote Uganda wamekuwa wakikumbushwa hiyo kamata kamata na funga ya wanyarwanda. Jibu limekuwa ni kuwazoa wafungwa walioteswa na kuwatupa kwenye mpaka wake na Rwanda. Kuanzia Januari 2018, wanyarwanda 1438 ndio waliotupwa kwenye mpaka wakitoka sehemu walizofungiwa kwa amri ya (CMI) au Idara kuu ya Upelelezi Uganda (ISO). Wengi wao hutupwa hapo wakiwa mahututi kutokana na mateso waliyofanyiwa.


Mwaka uliopita peke yake, waliotupwa mpakani ni 588 na 100 kati ya hao walitupwa mpakani kati ya mwezi Septemba na Disemba.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: